Waandishi wa habari mkoani Kagera wamehimizwa kutafuta sehemu maalumu za utunzaji wa kazi zao ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na utunzaji mbaya wa kazi zao.
Waandishi hao wameaswa hayo wakati wa mafunzo ya internet yaliyotolewa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA Tanzania katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambayo yametolewa kwa siku nne kwa waandishi 18 wanaotoka katika manispaa hiyo.
Wakati wa mafunzo hayo mwezeshaji kutoka katika Taasisi hiyo Bi FLORA RUGASHOBOROLA amesema kwa sasa watanzania wengi wanatumia mitandao ya kijamii hivyo ni rais mtu kuchukua kazi ya mwandishi katika mitandao ya kijamii endapo kazi hiyo haitahifadhiwa vizuri jambo ambalo linaweza kuleta matatizo kwa mwandishi.